Matangazo

HTML/JavaScript

Grand Grimoire, Joka Jekundu au Injili ya Shetani

Pichani ni Kitabu Kinachoitwa Grand Grimoire, Joka Jekundu au Injili ya Shetani. Kina Maombi ya Kumuita Shetani, Kumiliki Majini au Mali. Kanisa Katoliki Limewahi Kusema Kitabu Hiki Kipo Chini Yao na Halitaki Kiwafikie Watu. Kipo Tangu Karne ya 16.

Historia imeandika kuwa kitabu hiki kinaitwa Grand Grimoire, Red Dragon yaani joka jekundu au Gospel of Satan yaani Injili ya Shetani, inaelezwa kuwa kitabu hiki kiligunduliwa mwaka 1750 huko Yerusalemu Israel katika kaburi la Sulemani, kimeandikwa kwa lugha ya kiebrania na kispanyol.

Kitabu chenyewe kinadaiwa kuandikwa mwaka 1522 au nyuma zaidi, aliyekiandika anaitwa Antonio del Rabina kwa maagizo ya mfalme Sulemani, lakini kanisa katoliki limewahi kujitokeza na kusema kuwa lenyewe ndio lina umiliki wa kitabu hicho na halitaruhusu kukigawa kwa watu wapate kukisoma.

Lugha iliyoandikwa humo ni ya kueleweka kabisa, wataalamu wa mambo wanasema kuwa kitabu hicho kinapinga, kinasema kuwa mbinguni hakuna moto wala hakuna mateso yoyote, ni kitabu pekee chenye maarifa ya njia za kumwita shetani na kuwasiliana na na roho za giza kupitia sala zilizopo humo.

Humo pia kuna njia za kufanya ibada ya kuyaita mashetani yanayoitwa Puzuzu na mengine, na hata miujiza mbalimbali iliyoandikwa katika bibilia inadaiwa kupatikana katika kitabu hiki pia, na kuna njia za kufanya ibada maalumu.

Kitabu kimegawanyika katika sura mbili, sura ya kwanza inaitwa Secrum Regnum and Secrets, de L'Art Magique du Grand Grimoire, hapa kimelezea namna, Siri za namna ya kumrushia mtu pepo, siri ya uchawi NK.

Sura ya pili inaitwa Le Secret Magique où le Grand Art de Pouvoir parler aux Morts, hapa kinaelezea siri ya kuyaita mashetani na namna ya kufanya nayo maagano, kupata mali, kupendwa, kujifanya kama huonekani machoni pa watu NK.

full tazama video hii👇👇

https://youtu.be/3oELExSispE

No comments

Powered by Blogger.