Matangazo

HTML/JavaScript

maajabu ya mapiramids ya giza misri,wajenzi wake kumbe ni alien


Piramidi za Giza ni kati ya majengo yanayojulikana zaidi duniania  
yakoko kando ya bonde la mto Nile, karibu na mji wa Giza takriban kilometa 15 kutoka Kairo, mji mkuu wa Misri.

Historia ya maeneo ya makaburi ya Giza kwa jumla

Makaburi ya kwanza yalijengwa huko tangu chanzo cha milki ya Misri ya Kale takriban miaka 3,000 KK.



Piramidi kubwa na Sfinksi

Eneo la makaburi ya Giza hujulikana hasa kutokana na piramidi kubwa pamoja na sfinksi kubwa zilizokuwa maarufu tayari katika nyakati za kale. Mwanahistoria wa Ugiriki wa Kale aliyeitwa Herodoti alizihesabu kati ya Maajabu Saba ya Dunia na tangu siku zile miaka 2,500 iliyopita zilitembelewa na watalii.

Piramidi tatu kubwa zinajulikana kufuatana na majina ya Kigiriki ya mafarao au wafalme wa Misri : piramidi za Kheops, Khefren na Mykerinos. Piramidi za Kheops na Khefren ziko karibu kimo moja, ile ya Kheops ni kubwa kidogo lakini ile ya Khefren inaonekana kubwa kwa macho kwa sababu imejengwa juu ya ardhi ya juu kiasi kwa hiyo kwa macho ya mtazamaji inafika juu zaidi.

Jina la Kigiriki Jina la Kimisri Alitawala mnamo Kimo asilia Kimo cha leo Kipimo cha

upande wa msingi
Piramidi ya Kheops Khufru ~ 2620

- 2580 KK 146.1 m 138.75 m 230 m
Piramidi ya Khefren Khafre ~ 2558

-2532 KK 143.6 m 136.4 m 215.25
Piramidi ya Mykerinos Menkaure 2558

-2532 KK 65.55 m 62 m 102.2 m

x 104.4 m
Piramidi hizo zote hazikukaa peke yake bali zilijengwa pamoja na majengo ya kando.

Kila piramidi ilikuwa na mahekalu mawili ambako makuhani walitoa sadaka kwa ajili ya roho za mafarao marehemu peponi. Hekalu 1a kwanza lilijengwa mbali kidogo, kwenye chanzo cha barabara ya maandamano yaliyoendelea hadi hekalu la pili karibu na piramidi. Njia hizo za maandamano zilitumiwa hasa wakati wa sherehe za kumkumbuka farao.

Tangu siku za kale watu walichukua mawe kutoka majengo ya Misri kwa kuyatumia katika majengo ya nyakati zao. Hii ndiyo sababu ya kwamba kimo cha piramidi kimepunga na hasa mawe mazuri yaliyofunika nyuso za piramidi yamepotea.

Katika karne ya 12 BK mtawala wa Misri al-Malek al-Aziz Othman ben Yusuf alijaribu kubomoa piramidi akizitazama kama ushahidi wa upagani wa kale. Wafanyakazi walianza kukata mawe kutoka piramidi ndogo ya Mykerinos lakini ikaonekana ya kwamba kazi ya kubomoa labda ingekuwa ghali sawa na kujenga. Baada ya miezi kadhaa shughuli hizo zilisimamishwa na hadi leo kuna pengo katika baadhi ya mapiramids
lakini je wajenzi wa mapiramds haya ni akina nani?tazama video hii

No comments

Powered by Blogger.