Matangazo

HTML/JavaScript

MJUE MTU WA AJABU ALIYEITWA VANGELIA ALIYE TABARI KUTOKEA MATUKIO MENGI DUNIANI


Vangelia Gushterova - Vanga, alizaliwa tarehe 31 Mwezi wa Kwanza mwaka 1911 katika mji wa Strumica huko nchini Yugoslavia.
Akiwa na umri wa miaka 3, mama yake alifariki na pia baba yake alienda kupigana mstari wa mbele kwenye vita ya kwanza ya dunia, jambo lililomfanya Baba Vanga kubaki peke yake bila muangalizi.
Akiwa na umri wa miaka 7, baba yake alioa tena hivyo Vanga akapata mama mpya.
Mwaka 1923, familia yao ilihamia Novo Selo, huko Vanga aliishi maisha ya tabu na mateso sana.
Siku moja Vanga akiwa na binamu zake walienda tembelea chemi chem zijulikanazo kama Khan, wakiwa huko kulitokea kimbunga kikali sana ambacho kilomsomba Vanga na kwenda kumtupa kilomita kama 2 katikati ya shamba la mazao.
Akiwa yuko kwenye takataka na matope alihisi maumivu makali na alipofumbua macho aligundua kuwa haoni.
Zilifanyika juhudi za kumfanyia upasuaji mara tatu, ila alipofikisha umri wa mika 12 ilibainika kwamba hatoona tena hivyo akawa kipofu rasmi.
Alipelekwa akaishi kwenye makazi ya vipofu katika mji wa Zamun, mpaka alipofikisha umri wa miaka 18, ilipomlazimu kurudi nyumbani kuwalea wadogo zake baada ya mama yake wa kambo kufariki.
Hiki ndicho kipindi ambacho alianza tokewa na mambo ya ajabu kama kuota ndoto za ajabu, kupata maono, kuskia sauti, kuongea na watu waliokufa na mimea.
Pia alianza kutabiri matukio ambayo yalitokea kwa usahihi kabisa.
Ndipo jina la Baba Vanga likaibuka likiwa na maana Bibi Vanga katika lugha ya wa Bulgaria.
Alifariki tarehe 11 mwezi 11 mwaka 1996, na kabla ya kifo chake alisema kuwa kutatokea binti huko Ufaransa ambaye akiwa na miaka 10 ataanza kuwa mtabiri kama yeye.
Ametabiri matukio mengi yaliyotokea iliwemo kuibuka kwa ISIS, sept 11, kifo cha Stalin, Princess Diana kuza nyambizi ya Kirusi alitabiri hadi kwa jina ila mimi hapa chini nitaandika ambayo hayajatokea atakayependa kuona mengine akagoogle.
2016-
Waislamu wataivamia Ulaya na kufanya Uaribifu mkubwa kwa miaka mingi itakayofuata.
2018-
China itakuwa taifa lenye uchumi na ushawishi mkubwa duniani
2028-
Binadamu wataweza kwenda sayari ya Venus, pia kutatengenezwa chanzo kipya cha nishati tofauti na vyanzo vya sasa
2033-
Barafu zipatikanazo kwenye pembe za dunia zitayeyuka kwa kiwango cha juu na kusababisha bahari kuongezeka ukubwa kwa kula eneo la nchi kavu
2033-2046
Uchumi wa dunia utakuwa kwa kiwango cha juu, na Ulaya kutasimikwa utawala wa Kislamu.

Kufikia 2046, binadamu ataweza kufyatua (clone) viungo na hivyo kuwa na uwezo wa kutengeneza kiungo chochote katika mwili wa binadamu
2066-
USA itashambulia utawala wa Kislamu katika nchi za Ulaya kwa kutumia silaha mpya ya hali ya hewa itakayosababisha ubaridi wa kugandisha vitu hapo hapo.
2076-
Madaraja baina ya binadamu yatakuwa yamekoma na Ujamaa kupotea kabisa duniani.
2084-
Mfumo wa tabia nchi utajirekebisha na kujirudisha kama ulivyokuwa awali kabla ya uharibifu

2088-2097
Utaibuka ugonjwa mpya, ambapo binafamu anazeeka kwa kasi na dawa yake itapatikana 2097
2100-
Kutokana na jua letu kupungua nguvu, hivyo binadamu atatengeneza jua litakalo mulika upande wa dunia ambao utakuwa umekosa nishati ya hili jua

2100-2130
Binadamu watakuwa kama maroboti, na mwaka 2025, nchi ya Hungary itapokea ishara toka kwa viumbe wa anga za juu.
Kufikia 2130, viumbe hao watatembelea dunia na kusaidia binadamu kujenga makazi chini ya bahari.

2164-2200
Wanasayansi watafanikiwa kubadili wanyama kuwa nusu binadamu.
Kufikia 2170, kutatokea janga la ukame litakalosababisha njaa.


2183, moja wapo la koloni lililoanzishwa na binafamu huko sayari ya Mars, litakuwa na uwezo mkubwa wa siraha za Nyuklia hivyo kudai uhuru wake kutoka duniani.
2189, milipuko mikubwa miwili ya Volkano itazuiwa na mwaka 2195 binadamu watakaokuwa wameanzisha makazi chini ya bahari watakuwa wameweza kujitegemea kwa kila kitu hawatahitaji msaada wa aina yoyote toka juu au nchi kavu.
2200-2300
Sayari zitabadili njia zake za kuzunguka jua (orbits)
Kutaibuka binadamu wapya ambao watakuwa mchanganyiko wa weusi, weupe na njano.
Pia binadamu ataweza pata nishati kutoka katika vacccum (kiswahili chake sijui ila ni sehemu isiyo na hewa) na black holes(ni sehemu katika ulimwengu ambayo ina nguvu ya uvutano mkubwa kiasi kwamba kila kinachoingia hakiwezi kutoka hata mwanga. Hutokea pale nyota itapokufa na kugandamizwa)
Pia mawasiliano mapya yananzishwa na viumbe wengine wa anga za juu na binadamu atakuwa anauwezo wa kusafiri kwa kurudi miaka ya nyuma.

2300, jua litapoa na kushindwa kutoa nishati kabisa hivyo binadamu atatengeneza majua mengine kwa ajili ya nishati.
Pia sheria, kanuni na siri nyingi za ulimwengu zitajulikana.
Ajali itasababishwa na jua lililotengenezwa na mwanadamu na kuleta maafa ya ukame na njaa kali.
2480-
Majua mawili yaliyotengenezwa na mwanadamu yatagongana na kuiacha dunia katika giza totoro.

3000-4000
Vita kali itaibuka baina ya binadamu watakaokuwa wanaishi kwenye sayari ya Mars.

Jiwe kubwa litagonga mwezi na kusababisha vipande vya miamba kutengeneza pete itakayokuwa imezumguka dunia kama ilivyo kwenye sayari ya Saturn. ( japo kwa Saturn ile siyo miamba ni barafu)
Hili litayokea miaka 10 kabla ya kuanza kwa zama mpya.

3797-
Dunia itakuwa imeharibiwa vibaya kiasi cha kutokalika, ila binadamu watakuwa na uwezo wa kuishi katika sayari mbalimbali.
3800-
Binadamu wataamia kwa wingi katika sayari moja ambapo hali ya heea haitokuwa nzuri kwa ustawi wa viumbe wengine hivyo kutakuwa na mapigano ya kugombea rasilimali na nusu ya wakazi wa sayari hiyo watakufa kwenye hiyo vita.
Kufikia 3815, vita itaisha, maendeleo na ustaarabu utakoma na binadamu wataishi kama wanyama
3871-
Atatokea nabii mpya, atakayewahubiria watu kuhusu kutenda mema na kuhusu dini.
Watu wote watamuunga mkono na ataanzisha dini moja kwa watu wote.
3878, huyo nabii atawafunza kuhusu sayansi iliyosahauliwa.

4000-5000
Baada ya kuanza kwa zama mpya, miji mipya itajengwa na kutakuwepo maendeleo ya kisayansi.

4304, hakuna ugonjwa utakaokuwa hauna tiba
4308, binadamu watakuwa na uwezo wa kutumia 34% ya ubongo wao. Uovu na chuki itapotea baina ya binadamu.
4509, binadamu watamjua sana Mungu na watakuwa na uwezo wa kuwasiliana naye moja kwa moja.

4599, binadamu atakuwa na uwezo wa kuishi bila kufa.
4674, maendeleo yatakuwa yamefika kwenye kilele cha juu kabisa na kutakuwa na idadi ya watu bilion 340 walisambaa katika sayari mbali mbali.
Baada ya mwaka 5000, binadamu watakuwa wamefanya uamuzi wa kuvuka mipaka ya ulimwengu huu ambapo 60% watakubari na 40% hawatakataa.
5079, ulimwengu utafika kikomo.

No comments

Powered by Blogger.