FAIDA 11 ZA KIAFYA ZA MATUMIZI YA BANGI (MARIJUANA)
Katika baadhi ya nchi Duniani, matumizi ya bangi yamehalalishwa kuzingatia utashi wa mamlaka za nchi husika. Uruguy na Marekani (katika majimbo 20) ni mifano ya nchi hizo. Tafiti mbalimbali za kiafya zimefanyika na kupelekea ugunduzi kuwa bangi huweza kutumika kama tiba kwa baadhi ya magonjwa, isipokuwa haipaswi kutumika ovyo kama ilivyo kwa dawa zingine. Zifuatazo ni faida 11 za kiafya za bangi. Kisha tutaeleza na athari hasi za bangi hapo baadae.
1.Inaweza kutumika kukinga na kutibu presha ya jicho (glaucoma), bangi inapunguza presha ya jicho (intraocular pressure) kwa watu wenye presha ya kawaida na hata wale ambao presha ya jicho iko juu( glaucoma).
2. Inaweza kuboresha afya ya mapafu na kupunguza athari za tumbaku katika mapafu. Januari 2012, tafiti zilionesha bangi haiathiri kazi za mapafu badala yake huongeza ufanisi wa mapafu.
3. Huweza kuzuia kifafa. Kemikali aina ya Tetrahydrocannabinol au THC iliyopo katika bangi huambatana na seli za ubongo zinazochochea umeme katika mfumo wa fahamu. Muambatano huo hupunguza msisimko (excitability) wa mfumo w fahamu na kuzuia kutokea kwa kifafa.
4.Kuzuia kuenea kwa baadhi ya kansa, Cannabidiol au CBD ni kemikali iliyopo kwenye bangi ambayo hupunguza kuenea kwa kansa mwilini. Mfano, kansa ya matiti.
5.Inapunguza wasiwasi, maumivu na kichefuchefu, hata hivyo ikitumiwa kwa kiasi kikubwa huweza kuongeza wasiwasi.
6. Hupunguza na kutibu matatizo ya kutetemeka kwa misuli, (Parkinsonism)
7. Bangi huweza kutibu magonjwa ya utumbo (Inflammatory bowel diseases). Mwaka 2010 katika chuo cha Nottingham, tafiti ziligundua kuwa kemikali zilizopo kwenye bangi husaidiana na seli za mwilini kuongeza kinga za mwili na ufanisi wa utumbo.
8. Kupunguza maumivu ya viungo. Bangi hupunguza maumivu, hupunguza miwasho na kuleta usingizi.
9. Huboresha ngozi na kuchangamsha kazi za mwilini, Pia huongeza matumizi ya sukari mwilini.
10. Huongeza uwezo wa kubuni vitu(creativity), uwezo wa kukumbuka na uwezo wa kuzungumza.
11. Huweza kusaidia watu wanaopata matatizo ya mfadhaiko kutokana na kumbukumbu za mambo ya kutisha (post traumatic stress disorder) Mfano, Kwa wahanga wa majanga ya asili na yale yasio ya asili kama vita, moto, tsunami nk. Watu hao hupata kuona upya matukio ya kutisha walioshuhudia zamani na huweza pia kuyaona katika ndoto. Bangi huweza kuwasaidia kuepuka tatizo hilo. Maveterani wa vita ni mfano mzuri kabisa.
ANGALIZO. Matumizi ya kiafya ya bangi yanapaswa kuwa chini ya maelekezo ya mtaalamu/Wataalamu. Kwa kuwa athari zake hutegemea kiasi cha matumizi na hali ya afya ya mtumiaji. Inaaminika kuwa Bangi ina athari chache kulinganisha na pombe.
https://youtu.be/2vyXn5brdAg

No comments