Matangazo

HTML/JavaScript

FAHAMU HISTORIA YA KUTISHA JUU YA WATU KUZIKWA WAKIWA HAI

Watu wengi tumekua tusikia watu wakisimulia juu ya kuwa, kulikuwa na wafalme ambao walikuwa wakizikwa na watu waliokuwa hai, kama sehemu ya mila na tamaduni. Jamii ambayo ilifanya sana tamaduzi hizi ni Wakushi ambao walikuwa waafrika weusi waliopata kuishi katika falme ya Kinubia kuanzia miaka ya 1700-350 B.C.E( KABLA YA KIPINDI CHA UKRISTO).

Wafalme wa Kush walipokufa walikuwa wakizikwa takribani na wafuasi 300 waliokuwa hai, kama ishara ya kutoa sadaka kwa miungu yao.dhana ya kuzika watu hao ilihashilia kuwa binadamu anapokufa huwa kuna maisha mapya yaani Maisha Baada Ya Kifo, hivyo kwa kuwa aliyefariki alikuwa mfalme basi alipaswa kuzikwa na wafanyakazi wasiopungua 300 ili kumtumikia akiwa huko kaburini ambapo huko ndiko kuna maisha mapya.

Mfano wa mfalme wa Kush aliyezikwa na wafuasi zaidi ya 300 alikuwa mfalme Kashta aliyetawala kuanzia 760–747 B.C.E ( kabla ya kipindi cha Ukristo).sambamba na hilo makabuli yaliwekwa sehemu ya wazi ili kupata mwanga wa jua, kwani ikumbukwe kuwa Wamisri na Wanubia waliamini kuna maisha baada ya kifo. Na kwa mujibu wa Wanahistoria na wanaakiolojia wanasema kuwa Wamisri walikuwa na miungu yao mingi sana. Kwani kila sehemu ya maisha yao yalikuwa na mungu wake.

moja ya mungu wao alikuwa Jua (Sa-ra). Na asilimia kubwa ya wafalme waliokuwa wakizikwa, walizikwa kwenye sehemu zenye uwazi kama sehemu ya mahusiano ya karibu kati ya Watu waliokufa na miungu yao.

Na unaambiwa Kuwa kwa Wakati Ule kuzikwa ukiwa hai pamoja na mfame ilikuwa sifa kwa jamii na kwa familia pia. Yaani kuzikwa ukiwa hai ilikuwa ni moja ya ushujaa na baraka kubwa sana kwa wanajamii. Hivyo ikitokea Mfalme amefariki watu waligombania kuzikwa nae huku wakiwa hai.

No comments

Powered by Blogger.