Matangazo

HTML/JavaScript

FAHAMU MAZIKO YA KUSTAAJABISHA DUNIANI

MAZIKO YA KUSTAAJABISHA DUNIANI

1. Kabila la Dani kutoka bonde la Baliem Magharibi mwa Papua huko nchini New Guinea na mila za kukata vidole

Kwa upande wa kabila la Dani (au Ndani) ambalo linapatikana katika bonde la Baliem Magharibi mwa Papua huko nchini Papua New Guinea, wao ili kuonyesha huzuni mfiwa hukata kidole chake ambapo kitazikwa na mwili wa marehemu ili kuonyesha upendo kwamba alikuwa anampenda sana marehemu. hiyo inafanyika kama ni mume amefiwa na mkewe au mke amefiwa na mumewe au kufiwa na wazazi mtoto au ndugu wa karibu walioshibana kama kaka au dada.

Ukiona mtu wa kabila hilo ana idadi kubwa ya vidole vilivyokatwa hiyo inaonyesha amepata misiba mingi ya watu aliowapenda sana.

Hii mila ingekuwa huku kwetu na kwa jinsi tulivyokuwa na nasaba nyingi wengi tungekuwa hatuna kidole hata kimoja, maana ingetulazimu kukata hadi vya miguuni

2. Kabila la Yanomani kutoka katika nchi za Venezuela na Brazili na mtori uliochanganywa na majivu ya mwili wa marehemu,

Kwa kabila la Yanomani linalopatikana katika nchi za Venezuela na Brazili, hawa wakifiwa na ndugu wanauchoma mwili wa marehemu moto kisha yale majivu wanayachanganya na mtori na kisha kunywa kama ishara ya roho ya marehemu kuishi ndani mwao.

Imani hii imepewa nguvu sana kwa sababu kama isipofanyika hivyo wanaamini kwamba roho ya marehemu haitafurahi kwa kutelekezwa na hivyo itakuwa ikiwatafuta na kuwamaliza mmoja baada ya mwingine na ndiyo maana mtu wa kabila hilo akifa haraka haraka anachomwa na watu wanachanganya majivu yake na mtori wapate kumpumzisha mkatika matuombo yao na wao wabaki na amani ya bwana.

3. Wa-Tibet na Wamongolia na wanapogeuza matumbo ya Tumbusi kuwa makaburi ya wapendwa wao

Mila nyingine ya ajabu katika mazishi inaitwa Mazishi ya angani na hufanyika katika jimbo moja huko Uchina katika Jimbo la Tibet, Qinghai na nchini Mongolia ambapo mwili wa marehemu unakatwa katwa vipande na kuwekwa juu ya mlima ili mwili huo uliwe na wanyama au wale ndge walao mizoga maarufu kwa jina la Tumbusi (Vulture). Wanaamini kwmaba haina maana kuuhifandi mwili au kutumia ardhi vibaya kwa kuzika kasha tupu yaani mwili wa binadamu ambao utaharibu mazingira hivyo unwekwa eneo la wazi ambapo wanyama au hao ndege aina ya Tumbusi (Vulture) watajipatia msosi.

4. Wa-Fiji na mauaji ya mpendwa wao ili marehemu apate msindikizaji

Huko Katika visiwa vilivyopo kusini mwa bahari ya Pacific, nazungumzia visiwa vya Fiji, kama mtu kafa basi ndugu wa karibu ananyongwa ili marehemu asizikwe peke yake. Wanaamini kwamba marehemu ni lazima apte msindikizaji.

5. Wahindu na mila ya SATI, mwanamke kujitia kiberiti ili kufa kifo cha heshima baada ya mumewe kufa

Sati ni mila ya kale sana, kabla ya hizi dini zetu za mapokeo. Pale mume wa kihindu anapokufa, mkewe anatakiwa kwa hiyari yake mwenyewe ajitose kwenye moto uliowashwa ili afe kwa moto kwa heshima ya mumewe. Madhumuni ya mila hiyo ni kwmaba wahindu wanaamini kwamba wajane hawana nafasi hapa duniani baada ya waume zao kufa hivyo kwa heshima ya mumewe ni lazima mjane ajitose kwenye moto ili afe kishujaa...

No comments

Powered by Blogger.