Fahamu historia ya viongozi wa korea
Wakati wa uhai wake Kim Jong-il baba mzazi wa Kim Jong-Un, Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini alioa wanawake wawili ambao ni Hong Il-chon na Kim Young-sook. Lakini aliishi kinyumba na wanawake wengine watatu na kufanya jumla ya wanawake zake kuwa watano.
Hawa watatu hawakuwa wake wa ndoa bali mahawara, lakini waliotambulika rasmi na mamlaka za nchi hiyo (official domestic partners). Mahawara hao ni Song Hye-rim, Ko Yong-hui (mama yake Kiduku) na Kim Ok.
Mke wa kwanza aliitwa Hong il-Chong. Huyu hakuwa chaguo la Kim Jong-il bali chaguo la baba yake. Yani baba alimchagulia mtoto mwenzi ambaye alikua binti wa rafiki yake. Wakaoana mwaka 1966 na kuzaa mtoto mmoja (Kim Hye-gyong) lakini ndoa yao haikudumu. Mwaka 1969 wakatalikiana.
Baadae mwaka 1974 Kim Jong-il akaoa mwanamke mwingine aitwae Kim Young-sook ambaye nae alichaguliwa na baba yake tena. Japo ndoa yao ilikuwa na misukosuko mingi lakini waliishi pamoja hadi mwaka 2011 alipofariki. Alizaa nae mtoto mmoja aitwaye Kim Sul-song.
Kim Jong-il alianzisha mahusiano na wanawake wengine watatu kwa nyakati tofauti. Wa kwanza ni Song Hye-rim aliyezaa nae mtoto mmoja aitwaye Kim Jong-nam. Wa pili ni Ko Yong-hui aliyezaa nae watoto watatu ambao ni Kim Jong-chul, Kim Jong-un (kiduku) na Kim Yo-jong. Alikuwa pia na mahusiano na mwanamke aliyeitwa Kim Ok lakini hakuzaa nae.
Kim Jong-il alifanikiwa kupata watoto sita kwa wanawake wanne tofauti. Watoto wa kike watatu (Kim Hye-gyong, Kim Sul-song na Kim Yo-jong) na wa kiume ni watatu (Kim Jong-nam, Kim Jong-chul na Kim Jong-un).
Katika orodha hiyo mtoto mkubwa wa kiume ni Kim Jong-nam. Huyu ndiye aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kumrithi baba yake. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika wizara ya ulinzi ya nchi hiyo akiwa na umri wa maika 27 tu.
Mwaka 2000 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Tume ya sayansi na teknolijia ya nchi hiyo. Mwaka 2001 alifanya ziara nchini China na kupokelewa kwa heshima kubwa na serikali ya China na aliongoza jopo la mazungumzo kuhusu maendeleo ya teknolojia kati ya China na Korea kaskazini. Yote haya yalikuwa ni maandalizi ya kuja kuongoza taifa hilo la Kikomunisti kwa siku za baadae.
Lakini mwezi May mwaka 2001 alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Narita mjini Tolkyo, Japan kwa tuhuma za kuingia nchini humo akiwa na hati ya kughushi (fake passport) ya Jamhuri ya Dominica. Tukio hilo lilisababisha mgogoro kati ya Korea kaskazini na Japan na kusababisha kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-il kuahirisha safari yake aliyokua ameipanga nchini Japan.
Baaada ya tukio hilo Kim Jong-Nam alianza kupoteza ushawishi kwa baba yake na kuonekana hafai kushika madaraka ya juu ya nchi hiyo. Mwaka 2003 aliondoka Korea Kaskazini na kuamua kwenda kuishi mjini Macau nchini China. Akiwa huko alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kwamba hana mpango wa kurithi nafasi ya baba yake kama wengi wadhaniavyo.
Alisema kuwa matamanio yake ni kuona Korea kaskazini inafanya mabadiliko ya kimfumo na kuachana na ukomunisti, badala yake iruhusu uchumi wa soko huria, demokrasia, uhuru wa habari, utawala wa sheria etc. Akaongeza kuwa ukomunisti umeifanya nchi hiyo kujifungia kwenye chumba cha peke yake wakati huu ambapo dunia nzima inaamini katika utandawazi.
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mtoto kutoka ukoo wa Kim kuongea na vyombo vya habari nje ya Korea kaskazini. Hivyo ‘press’ hiyo ilizidi kumpotezea umaarufu na kukawepo na uvumi kwamba amekua wakala wa shirika la Ujasusi la Marekani CIA.
Jarida la Wall Street Journal liliandika kwamba kuna ushahidi wa mawasiliano kati ya Kim Jong-Nam na CIA kwa kipindi kirefu tangu alipokua anasoma Uswisi. Jarida hilo lilieleza kuwa hata mjini Macau alikokuwa akiishi alikuwa amepewa ulinzi na CIA na alikuwa akitumia nyaraka bandia ili kuficha utambulisho wake. Lakini madai hayo hayakuwahi kuthibitishwa popote.
Mwaka 2006 aliponea chupuchupu kuuawa kwa risasi katika uwanja wa ndege wa Budapest Ferihegy nchini Hungary. Tangu wakati huo ameshaponea majaribio kadhaa ya kuuawa katika maeneo na miji tofauti. Mwaka 2007 mamlaka mjini Pyongyang zilidai kwamba Kim Jong-Nam alikuwa na pasi ya kusafiria ya Ureno lakini Ureno ilipinga madai hayo na kusema labda awe ameghushi.
Mwaka 2003 baada ya Kim Jong-Nam kuonekana hawezi kupewa nafasi ya kurithi uongozi, Jeshi la nchi hiyo likaanzisha kampeni ili urithi uende kwa mmoja kati ya watoto watatu wa Ko Yong-Hui. Walijua Ko Yong-Hui alikua kipenzi cha Kim Jong-il hivyo asingeweza kukataa.
Ko Yong-Hui alipendwa na jeshi la nchi hiyo, na walimpachika jina kuwa mwanamke anayeheshimika zaidi nchini humo na mtiifu zaidi kwa kiongozi mkuu wa taifa hilo (The most respected Mother and the Most Loyal subject to the Supreme Leader).
Ushawishi huo ukazaa matunda. Mwaka 2004 Kim Jong-il akaanza kumpangia kazi mwanae mdogo wa kiume Kim Jong-Un na kumuweka karibu na serikali akiwa kijana mdogo wa miaka 20 tu.
Mwaka 2004 Kim Jong-il alipofanya ziara China alikaimisha uongozi wa nchi hiyo kwa mwanae mdogo Kim Jong-Un. Kwahiyo "kiduku" akaongoza nchi hiyo kwa zaidi ya wiki moja hadi baba yake aliporudi kutoka China. Na mwaka 2010 mzee akatangaza rasmi kwamba Kim Jong-Un ndiye mrithi wake.
Mwaka 2011 baada ya kifo cha baba yao Kim Jong-Nam alienda Korea kaskazini na kukutana na mdogo wake Kim Jong-Un kwa mara ya kwanza (Hawakuwahi kukutana kabla kwa sababu ya kulelewa mazingira tofauti).
Hata hivyo Kim Jong-Un alimuona kaka yake kama "threat" kwenye urithi wa kiti cha uongozi wa nchi hiyo, hivyo alipanga kumuua baada tu ya mazishi ya baba yao. Kim Jong-Nam "aliposhtukia" akaondoka na kurudi China kabla ya mazishi ya baba yao. Hakumzika baba yake kwa kuhofia maisha yake.
Baada ya mazishi Kim Jong-Un alisimikwa rasmi kuwa Kiongozi mpya wa taifa hilo, lakini aliendelea kumsakama kaka yake Kim Jong-Nam na kumuwekea mitego mingi ya kumuua. Mwaka 2012 shushushu mmoja wa Korea kaskazini aitwaye Kim Yong-su alikamatwa huko China na kukiri kwamba walikuwa kwenye mpango wa kumuua Kim Jong-Nam kwa maelekezo ya mdogo wake Kim Jong-un.
Kim Jong-Nam aliamua kumuandikia mdogo wake barua kumuomba asimdhuru na kwamba hakuwa na mpango wowote na madaraka ya nchi hiyo. ‘Tafadhali naomba usinidhuru. Kumbuka sisi ni ndugu wa damu, na hakuna nilipokukosea? Kama ni uongozi wewe ndiye uliyeachiwa dhamana na unazo baraka zote kutoka kwangu’. Sehemu ya barua hiyo ilinukuliwa katika kitabu chake kiitwacho ‘My Father Kim Jong-il, and Me’ kilichoandikwa na mwandishi Yōji Gomi wa nchini Japan.
Lakini February 13 mwaka 2017 Kim Jong-Nam akiwa uwanja wa ndege wa Kualar-Lumpar, Malaysia akisubiri ndege kurudi Macau, alifuatwa na wasichana wawili wakiwa wamevalia ‘gloves’ na mmoja akamshika usoni kisha wasichana hao kutoweka.
Dakika chache baada ya tukio hilo hali yake ilianza kubadilika na alipokimbizwa hospitalini alifariki dunia. Vipimo vilionesha kwamba alinusa sumu aina ya VX (nerve agent) inayoaminika kuwa hatari zaidi na yenye kuua haraka.
Picha za CCTV uwanjani hapo ziliwaonesha wasichana hao na waliweza kutambulika kuwa ni Siti Aisyah raia wa Indonesia na Doan Thi Huong raia wa Vietnam waliokua wakifanya kazi kwenye kampuni moja ya masoko mjini Kualar Lumpar. Walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji.
Walijitetea kwamaba siku chache kabla ya tukio hilo walifuatwa na wanaume wanne na kuwapa offer ya kucheza mchezo wa kushtua watu uwanjani hapo (prank). Walikubali na wakafanya ‘prank’ hiyo siku ya pili yake.
Lakini kesho yake walifuatwa tena na wanaume hao na kuambiwa wavae "gloves" kisha wakapewa "poda maalumu" na kuelekezwa wakamshike usoni abiria mmoja aliyekuwa akisubiria ndege uwanjani hapo. Walifanya hivyo wakijua ni ‘prank’ kumbe walisababisha mauaji. Wanaume hao waligundulika baadae kuwa ni majasusi kutoka Korea kaskazini.
Mahakama ilizingatia utetezi huo na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuua bila kukusudia. Hata hivyo mwezi Machi mwaka 2019 waliachiwa huru baada ya kupunguziwa theluthi moja ya vifungo vyao.
Unaweza kusoma zaidi simulizi hii na nyingine nyingi kwa kununua kitabu cha ISTILAHI ZA UHALIFU NA USALAMA. Kinapatikana House of Wisdom Bookshop, Posta. Au piga simu 0713933736 au 0745830775 kuletewa popote ulipo.!

No comments