Matangazo

HTML/JavaScript

Fahamu tafsiri ya ndoto za kupaa

TAFSIRI YA KUOTA NDOTO ZA KUPAA HEWANI

Amani iwe juu yenu

leeo nawapa tafsiri ya ndoto hii ya kupaa au kuruka na kwenda hewani

Ndoto hii huotwa sana na watu wenye ustaarabu au wapole na wenye dalili za mafanikio au wenye mipango mikubwa inayokwama

Kuota unapaa kama wewe ni mtegemeaji kazi za vibarua na kazi za kuitwa ukiiota mara moja ndoto hii utaitwa kazini au kibaruani

Kuota ndoto hii mara moja ni dalili ya kufanikiwa

Kuiota mara kwa mara ni dalili ya kusumbuliwa na jini subiani mbaya na huyu huwa katika kundi la jini mahabba hapa ndo utaona mambo hayaendi yamekwama kila ufanyalo huushia kupata hasara

Ndoto hii pia huiota mtu mwenye kuumwa mara kwa mara na hasa wale wanaoumwa sana vichwa miguu na mikono

Ndoto hii unapoiota unakimbizwa kisha ukapaa ni dalili ya kumshinda mpinzani wako au adui yako

Kadhalika kuiota unakimbizwa na mbwa au simba ni dalili ya uadui lakini utaushinda uadu huu

Ndoto hii ni ndoto nzuri na mbaya

Nzuri ukiiota mara moja moja

Mbaya ukiiota mara kwa mara.

No comments

Powered by Blogger.