Taifa la Sweden lina mambo mengi ya kushangaza. Umewahi kuyasikia haya kuhusu Sweden?

1.Kila mmoja anaruhusiwa kukwea jukwaa harusini.

harusi

Atakaye kuzungumza anaweza hata iwapo sio sherehe yake ya harusi.

Kwa kawaida, ingawa kwenye sherehe za ndoa, ni baba, mama, au wazazi wa wanandoa pekee huruhusiwa kuzungumza, ni hali tofauti Sweden. Kila mtu anakaribishwa kuropokwa.

Jamaa wa karibu wa wanandoa, wakiwemo marafiki, majirani na yeyote, mwenye semi za kusema, anapewa nafasi kwenye jukwaa.

Hata hivyo sio kazi rahisi kwani hili husababisha sherehe za harusi kuendelea hadi saa sita za Usiku.

Hata kama huna la kusema, unakabidhiwa zamu urushie mawili matatu ya kuwafurahisha au kuwaliza waalikwa kwenye hafla ya harusi.

Aidha, ndoa za Sweden hazina mtu aliyechaguliwa kuandamana na bi harusi au bwana harusi kwani wanahisi na kuamini sio muhimu.

2. Wototo hula peremende pekee siku ya Jumamosi

Peremende

Ingawa raia wa Sweden wanaongoza kwa ulaji wa peremende duniani, watoto wa taifa hilo, hawajaathiriwa na uharibifu wa meno.

Siku ya Jumamosi nchini Sweden inafahamika kuwa "Lördagsgodis" au "Jumamosi ya peremende".

Tamaduni hizi zimeanzishwa miaka ya 1940s na '50s na madaktari wa meno wa taifa hilo.

Kulingana nao, ni vyema kwa afya kula sukari ya wiki ndani ya siku moja kuliko kula vipimo vidogo kila siku katika wiki.

3. Hawapendi pesa.

Image copyrightGETTY IMAGESPesa

Ingawa pesa ni kitu chenye thamani, kwa raia wa Sweden, ni karatasi zisizo na maana.

Vilevile, pesa taslimu hazitumiki kila sehemu.

Mikahawa, na hata maduka huruhusu kadi pekee.

Hata benki hazimhruhusu mtu kutoa au kuweka pesa zake.

Hata mafukara wa Sweden wamejihami na mitambo ya kadi ya benki kwani hakuna anayewapa pesa.

Hii ni kwa sababu wanaamini kuwa hali hiyo inapunguza viwango vya uhalifu.

Hata mwimbaji wa wimbo 'Money Money Money - wa kundi la ABBA, Björn Ulvaeus, amekuwa akiishi na kutembea bila pesa tangu mwanawe alipoibiwa pesa zake na majambazi.

4. Wanafunzi hupiga nduru kila usiku

Mtu anayepiga kelele

Kila mtu anayelenga kusoma, Mazingira anayoyastahili ni tulivu na yasiyo na kelele.

Hapa Sweden ni kinyume kabisa.

Pindi wanafunzi wanapochoka kusoma au wanahitahi mapumziko mafupi baada ya muda mrefu wa kusoma, wanaruhusiwa kutoka nje na kupiga kelele.

Kila usiku ifikapo saa nne za usiku, Wanafunzi katika chuo kikuu cha Uppsala, wanapewa nafasi katika barabara moja iitwayo Flogsta ambapo wanatoka nje na kupiga mayowe.

"nduru za Flogsta" zimeenea hadi vyuo vingine taifa hilo.

5. Ni marufuku ''kuomba kupunguziwa bei ya pombe'' Sweden

Vinywaji

Uhusiano wa Waswidi na pombe sio wa kuzungumziwa.

Yaani, imefika kiwango ambacho walilenga kupiga marufuku mnamo 1920.

Baada ya Marekani kupiga marufuku unywaji pombe, Sweden nayo iliitisha kura ya maoni.

Ingawa kura hiyo ilishindwa na waliopinga kuzuiwa kwa pombe wakiongozwa na msanii Albert Engström, aliyewaambia raia kuwa iwapo ingepigwa marufuku, hawangejivinjari walivyozoea.

Tangu hapo, uuzaji wa pombe umegubikwa na sheria kali zinazolenga kupunguza utumiaji wake.

Ni marufuku kufanya 'ofa' za pombe au hata matangazo ya kupunguza bei.

Haya yanalenga kuzuia uwezekano wa pombe kuwavutia watu na kuishia kutumia vinywaji hivyo.