Matangazo

HTML/JavaScript

FAHAMU TABIA ZA NYOTA ZAKO KATIKA MAPENZI

TABIA ZA NYOTA YAKO KATIKA MAPENZI

Katika mapenzi kila mmoja amekuwa na tabia ya aina fulani lakini kwa wale wanaoamini masuala ya nyota wanasema kuwa nyota hueleza tabia za mtu katika maisha yake halisi , na hizi ndo tabia za wewe uliyezaliwa leo kwenye mapenzi



PUNDA


Punda ni wakali na wachangamfu, wenye hisia na wanaoweza kujieleza wakiwa na ari ya kufanya chochote. “SASA HIVI” hayo ndio mambo wanayotaka kusikia.
Ni watu wasiokuwa na subira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu, wakati wote wanajiona kwamba “Wanajua sana”.
Kwa ujumla wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kubwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia katika mapenzi bila kufikiri, wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu


MAPACHA
Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Katika mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.

0653 532036 whatsapp
0764 995259

No comments

Powered by Blogger.