Mjue mansa Musa mfalme aliyekuwa tajiri kutoka afrika
UNAMFAHAMU MANSA MUSA? BINADAMU TAJIRI ALIYEPATA KUISHI MIAKA YA 1280 -1337
UNAMFAHAMU MANSA MUSA? BINADAMU TAJIRI ALIYEPATA KUISHI?
Mimi binafsi napenda kumuita Mansa Kankan Musa I, alipata kuishi mwaka 1280 hadi mwaka 1337 japo kuna vyanzo vingine vimekataa hilo na kudai alifariki mapema zaidi..
Mansa Musa I anasadikika kuwa miongoni mwa watu tajiri zaidi katika historia! mtupilie mbali J.D. Rockerfeller! Mansa Musa, alipata kuwa "mansa" yaani mfalme wa wafalme, katika ufalme mkubwa wa afrika ya kabla ya ukoloni ulioanzishwa na mtu aliyepata kuitwa Sundiata Keita, "Malike Empire" au Mali Empire.
Mansa Musa aliweza kuudhihirishia ulimwengu na ni kielelezo tosha cha kuonesha kwamba afrika sio bara masikini na halikuwa bara giza, mnamo mwaka 1324 alipoenda kuzuru makkah kwa ajili ya ibada ya waisilamu ya hijja!
Mansa Musa alifanya safari ya KIHISTORIA iliyobaki kuwa mazungumzo kwa wanafunzi wa historia hadi leo hii, kwa kuonesha fahari iliyotukuka ya ardhi ya neema ya madini ya Mali kwa kubeba waungwana 60,000 pamoja na watumwa 12,000 pamoja nae ambao walibeba pound 4 za dhahabu kila mmoja na ndani ya msafara kulikuwa na ngamia 80 waliokuwa wamevishwa mavazi ya thamani na kubebeshwa mifuko ya unga wa dhahabu kadiri ya pound 50 kwa 300 kila mmoja..
Mansa Musa alipita akigawa dhahabu kwa masikini kuanzia Mali hadi Misri alipotua, kisha kuvuka maji na kuingia saudia akiwa amejizatiti.. aliweza kuzifanya nchi za Saudia na Misri kushuka kiuchumi hadi anakufa, miaka kumi na kitu baadae, kwani bei ya dhahabu ilishuka sana na kupoteza thamani kwani ilikuwa ya kumwagaa!! Alitoa kiasi kikubwa zaidi cha pesa kama zawadi kwa Sultan wa wakati huo wa Misri na Saudia. pia katika safari yake hiyo aliweza kujenga misikiti kila alipokuwa njiani ilikuwa ni desturi yake kujenga misikiti kila ijumaa, baadhi ya misikiti ambayo ipo hadi leo hii!
Musa alirithi ufalme kutoka kwa Abubakari II ambaye alikufa maji katika bahari ya atlantic alipojaribu kuvuka kuona upande wa pili wa dunia, akiwa na boti zaidi ya mia mbili!! zilizosheheni vyakula na maji kwa ajili ya safari ya miaka kadhaa kufika mwisho wa bahariii.............!!
Jina mansa musa sio jina geni hata kabla ya maijilio ya wazungu, wana historia wengi kama Ibn Battuta wamemuelezea Mansa Musa hata kabla ya ukoloni mkongwe....Arabia, Europa, Israel na west Indies wote wameandika vitabu na vitabu juu ya tajiri huyu.........
Lakini Propaganda za wengi zimefanya nchi kama Mali, leo hii ni ya kupewa misaada kwa sababu ya machafuko ya kushinikiza..hii ni nchi iliyotukuka hata kabla ya kugundulika bara la Amerika karne ya 15.
NANI ANASEMA AFRIKA TULIKUWA MANYANI KABLA YA WAZUNGU?
NANI ANASEMA AFRIKA HAINA HISTORIA ZAIDI YA GIZA?
NANI ANASEMA AFRIKA HAIKUWA NA MAENDELEO?
NANI ANASEMA TULISHINDWA KUJITAWALA?
NANI ANASEMA HATUKUTAMBULIKA DUNIANI?
NANI ANYOOSHE KIDOLE..........!!!
Jifunze maarifa ya ukweli!!