TAFSIRI NDOTO ZAKO MWENYEWE part (1)
TAFSIRI NDOTO ZAKO MWENYEWE[SEHEMU YA KWANZA]
MWANAMKE UKIOTA UNA NDEVU
Mwanamke ukiota una ndevu ni dalili ya kuwa hutazaa milele,na baadhi ya wafasiri wamesema ni dalili ya maradhi ambayo yatampata siku za usoni,au ziada ya mali ya mumewe na utukufu wa mwanawe wa kiume.
KAMA AKIWA AMEOLEWA
Ni ishara ya mumewe kuondoka
AKIWA NI MJAMZITO
Atazaa mtoto wa kiume na litatimia jambo lake
AKIOTA NDEVU ZIMEREFUKA NA KUWA NYINGI
Umri wake utakuwa mrefu na mali yake itazidi kuongezeka
UKIOTA UNA MASKIO MATATU
Ni ishara ya kuwa na mke mmoja na mabinti wawili
UKIOTA UNA SIKIO NUSU
Inajulisha kifo cha mkeo na kuwa utaoa mwingine badala yake
UKIOTA UNA MASKIO MANNE
Inajulisha moja kati ya mambo mawili
1.utakuwa na wake wanne
2.mabinti wanne wasiokuwa na mama
UKIOTA MASKIO YAKO YAMEJAZWA VITU NDANI YAKE
Ni dalili ya kuwa utakufuru
KUOTA MENO YANAVUNJIKA
Ni dalili ya kuwa utalipa deni lako kidogokidogo
UKIOTA MENO YANADONDOKA NA UNAHISI MAUMIVU
Ni dalili ya kuondokewa na kitu katika vitu vilivyomo ndani mwako
UKIOTA MENO YAKO YA MBELE TUU YANADONDOKA
Ni dalili ya kuwa unazuiwa kufanya jambo lako ulilokuwa ukilifanya ima kwa vitendo au maneno
UKIOTA KITU KINATOKA MDOMONI MWAKO
Ni dalili ya rizki utakayoipata iwe ni halali au haramu
UKIOTA UNA ULIMI MREFU
Ni dalili ya kushinda katika ufasaha wa kuongea na adabu yako,upole na utukufu
UKIOTA ULIMI WAKO UMEFUNGWA
Ni dalili ya ufukara na maradhi
UKIOTA UNA MENO MEUPE NA MAZURI
Ni dalili ya ziada katika nguvu na mali ya daraja ya juu kwa watu wa nyumbani mwake
UKIOTA UNA MENO YA DHAHABU
ukiwa ni mwenye elimu basi ndoto yako ina sifa nzuri,na ikiwa sio mwenye elimu basi basi ni dalili ya shari na watu wako watapatwa na maradhi au kuangamia
UKIOTA UNA MENO YA FEDHA
Ni dalili ya kupata hasara katika mali yako,na yakiwa ni meno ya kioo ni dalili ya umauti
KUOTA UNALISHA MASKINI
Utatoka kwenye majonzi na utapata amani kama ulikuwa na hofu
UKIOTA UNASWALI KATIKA ALKAABA
Utapata baadhi ya watukufu na viongozi na utapata amani na kheri
UKIOTA UMEKUFA NA KUFUFUKA
Utafanya madhambi na utamuomba mungu msamaha
KUOTA UNAKUFA BILA KUUMWA
Umri wako utakuwa mrefuu
UKIOTA UMEKUFA,WATU WANAOMBELEZA NA KUKUFANYIA SHUGHLI ZA MAZISHI
Dunia yako itakuwa nzuri lakini akhera yako imeharibika
KUOTA MAITI INAJIOSHA YENYEWE
Watu wako watatoka kwenye majonzi na mali yao itazidi
KUOTA UNAONA SANDA
NI DALILI YA ZINAA
UKIOTA SANDA IMEVESHWA LAKINI HAIJAKAMILIKA UVAAJI WAKE
Utatiwa kwenye zinaa lakini hutokubali
UKIOTA UMEFUNGWA KWENYE SANDA VILEVILE KAMA MAITI
Ni ishara ya kifo chako
KUOTA UPO KWENYE JENEZA
Utajenga udugu na mtu kwa ajili ya mungu
UKIOTA UPO KWENYE JENEZA NA WATU WAMELIBEBA
Utatawala na kupanda daraja na watu watakufuata kama ulivyowaona ndotoni
UKIOTA UMEBEBA MAITI
Utapata mali ya haramu
UKIOTA UNAMPELEKA MAITI SOKONI
Utapata mahitaji yako na faida kwenye biashara zako
UKIOTA JENEZA LINAPITA HEWANI
Atakufa mtu mkubwa kama rais,mwanachuoni au yeyote mwenye daraja ya juu
UKIOTA UMEKUFA NA UNAZIKWA
Utasafiri safari ya mbali na utapata mali
KUOTA UMEMFUFUA MAITI
Utamsilimisha mtu wa dini nyingine kuwa muislam au mtu muovu atatubia dhambi zake kwako
UKIMUOTA DADA YAKO ALIYEKUFA ANAISHI
Utajiwa na mgeni kutoka safarini na utafurahi
UNGANA NAMI KATIKA SEHEMU YA PILI
No comments