Matangazo

HTML/JavaScript

DARFUR ; ZIMWI LA KUTENGENEZA LENYE KUITESA TAIFA LA SUDAN.

DARFUR ; ZIMWI LA KUTENGENEZA LENYE KUITESA TAIFA LA SUDAN.



Darfur ni jimbo huru linalotawaliwa na Sudan tangu mwaka 1916. Mzozo wa Darfur unajumuisha udini, siasa na maslahi ya kiuchumi hasa mafuta ya Darfur,ni mzozo wa kidini kati ya Waislamu waarabu na Waislamu waafrika kwenye eneo la waafrika ambao wanadhulumiwa maeneo yao na Waarabu wenye nguvu ya kijeshi na dola.

Mkoa wa Darfur unapatikana Magharibi mwaka taifa la Sudan, kiujumla mkoa wa Darfur una majimbo matano ambayo ni central Darfur, East Darfur, North Darfur, South Darfur na West Darfur.

Makadilio ya watu ni zaidi ya million 10, huku asilimia 98 wakiwa ni Waislamu. Ambao wanabaguana, kuuana, kutengana na kutosaidiana kwa vigezo vya rangi, chuki za kutengeneza na mambo ya kijasusi na kijeshi.

Historia ya Darfur ni ya zamani sana, watu weusi yaani waafrika ndio wenyeji wa Afrika kaskazini tangu mwaka 10,000 K.K, nchi za Libya, Morocco Algeria, Tunisia na Misri zilikaliwa na waafrika kwa miaka mingi na baadae waarabu walivamia wakitokea sumeria na Palestina. Uvamizi wa waarabu Afrika ya kaskazini ukaanza kubadilisha historia na urithi wa watu weusi hasa jamii ya Wanubi au Kemeti.

Ustaraabu wa kwanza wa eneo la Darfur ulianza karne ya 12 ambapo kabila la Daju liliweka makazi eneo la Darfur na kusimamisha himaya yenye nguvu mpaka eneo la Kordofan.Utawala wa Daju ulijikita kwenye kilimo, biashara na teknolojia ya chuma. Daju wakishirikiana na jamii za watu wa jangwa la Sahara hasa Bedouin na Berbers ili kumudu mazingira yao.

Baadae wakaja watu wenye nguvu wa Tunjur ambao walipigana na Daju kuanzia mwaka 1230_1340 hatimae Daju wakapigwa na kuhamia maeneo ya Abyei, Denga, Darsila na Mongo maeneo hayo kwa sasa hivi ni Chad.

Watawala wa Tunjur wakaona na kufanya ushirika na Fur hasa kiongozi wao Mussa Sulayman (1609_1695) huyu alikuwa kiongozi Mkuu wa Darfur. Neno Darfur ni neno la kiarabu "Dar "lenye maana ya nyumba au jengo wakati neno Fur ni kabila la wazawa wa Darfur hivyo basi Darfur maana yake ni nyumba ya wafur.

Fur ni mojawapo ya jamii za Kemeti ambao ni waafrika wenyeji wa Misri, Sudan na Libya.

Darfur iliendelea kuwa jimbo huru Magharibi mwa Sudan huku ustaraabu wa watu wa Darfur ukitaradadi kiuchumi, kisiasa, na kiutamaduni, enzi hizo hakukuwa na Waarabu eneo nzima la Darfur, walikuwa ni waafrika peke yao. Enzi hizo waarabu waliishi pwani hasa Khartoum na Suaqini.

Mwaka 1875 Darfur ilivamiwa na Waarabu wa Misri kupitia Khartoum, miongoni mwa wavamizi hao alikuwepo nguri wa biashara za magendo hasa utumwa, pembe za ndovu na ngozi za wanyama bwana huyo aliitwa AL Zubayr Rahman Mansour Pasha (1810-1900).

Ambaye alisafiri kutoka Mashariki ya kati, kupitia Misri, Khartoum Sudan mpaka Darfur kutafuta watumwa na pembe za ndovu.

Waislamu wa Darfur waliungana kupambana na wavamizi hao wa Kiarabu kutoka Misri na dola ya kiislamu yaani Ottoman Empire.

 Viongozi hao wa Darfur waliongozwa na mashehe, maimamu na baadhi ya wanazuoni wenye uzalendo na eneo la Darfur. Baadhi ya wapiganaji walikuwa ni Sultan Mahdi wa Darfur, Muhammad Ahmad, na Sheick Madibbo kwa pamoja walishinda vita hivyo dhidi ya Generali Slatin Pasha wa Misri.

Baadae Ottoman Empire na viongozi wa Darfur wakakubaliana kwamba Darfur ibaki kuwa huru na Ottoman Empire watatawala eneo la Khartoum na Misri

hivyo Dola ya Kiislam iliwapa uhuru waafrika wa Darfur baada ya kuona fikra zao na ushujaa vitani, mnyukano wa Aya na hadithi za kiislamu ulikuwa mkubwa wakati wa makubaliano hayo ya uhuru wa Darfur, kumbe baadhi ya Waarabu wa Khartoum roho iliwauma Darfur kuwa huru.

Mwaka 1916 Ottoman Empire walipigwa vibaya sana na wakapewa masharti ya kuondoka Sudan, hivyo Jeshi la Uingereza likashirikiana na Waarabu wachache wa Khartoum kuiteka Darfur kuanzia hapo wananchi wa Darfur wakaanza kupoteza uhuru wao na ustaraabu wao wa Darfur uliodumu kwa zaidi ya miaka 10,000.

Sudan ilipata uhuru tarehe 1/1/1956 chini ya Ismail AL Azhari (1900_1969) huyu alikuwa mwafrika na msomi kutoka Khartoum na alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Sudan kuanzia mwaka 1954_1956 na baadae raisi wa tatu wa Sudan kuanzia mwaka 1965_1969 ambapo alipinduliwa na mwarabu aliyeleta udini ubaguzi wa rangi na ukanda Generali Gaafar Nimeiry (1928_2009)  huyu alikuwa raisi wa Sudan kuanzia mwaka 1969_1986.

Utawala wa Gaafar Nimeiry ulijikita zaidi kupanua sera za waarabu yaani Pan Arabism movement, hivyo eneo la Darfur alitaka wachukue wafugaji wa Kiarabu huku waafrika wa Darfur ambao kiasili ni wakulima alitaka wawe vibarua na vibaraka wa waarabu.

Labda Generali Gaafar Nimeiry atakumbukwa kwa ujanja ujanja alioufanya mwaka 1983 baada ya kutoa amri kwa Jeshi la Sudan kuvunja viwanda vya pombe nchi nzima na pombe yote stoo kumwagwa kwenye mto Nile

Mwaka 1977 Generali Gaafar Nimeiry alianza mchakato wa kuuza mafuta ya Darfur, Kordofan na Khartoum kwenye makampuni makubwa kutoka Uingereza, Ufaransa, Marekani, China, India na Urusi, katika mchakato huo wa kuuza mafuta hakuna viongozi wa Darfur walioshirikishwa kuanzia hapo Darfur na Khartoum kukawa nongwa na chuki.

Cha kustaajabisha ni kwamba makampuni hayo yalitoa ajira nzuri kwa waarabu wa Khartoum huku wazawa wa Darfur wakiwa kama vibarua. Generali Gaafar Nimeiry aliungana na Rais wa Libya Muammar Mohammed Abu Minyar Gaddafi (1942_2011) viongozi hao walikuwa wanaunga mkono harakati za makundi mbalimbali ya Kiarabu jangwa la Sahara hasa wafugaji ikiwemo Bedouin, Berbers, Aggbara na makundi mengine ambayo yalikuwa yanapora ardhi za wakulima ambao ni waafrika.

Ushirika wa Gaafar Nimeiry na Muammar Gaddafi ulisababisha ukabila, ukanda na vita za ardhi kwenye nchi zifuatazo Mali, Sudan, Chad na Libya.

 Katika eneo la Darfur makabila ya Kiarabu yakaanza kujitanua na kuanza kuchukua maeneo ya waafrika, waarabu wengi wafugaji walianza kuhamia Darfur huku wakipewa kinga na Generali Gaafar Nimeiry.

Mwaka 1986 wananchi wa Sudan waliandamana usiku na mchana kupinga utawala wa kijeshi wa Generali Gaafar Nimeiry na baadae nguvu ya umma ikashinda na hatimae dikteta Nimeiry akajiuzulu hivyo Bunge la Sudan likamchagua kiongozi wa chama cha Umma party Ustadhi Alhaji Profesa SADIQ EL MAHDI ambaye aliongoza nchi ya Sudan kiungwana na kidemokrasia huku eneo la Darfur akipanga kulipa uhuru lijitegemee kisiasa na kimaamuzi.

Mpango huo ulifeli baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan yalioandaliwa na Brigedia Generali Omar AL Bashir ambaye alikuwa Raisi wa Sudan kijeshi kuanzia mwaka 1989 mpaka mwaka 2019 ambapo maandamano ya umma yalimtoa madarakani.

Omar Bashir akaanza kuwa kinyume na mabeberu kwenye mafuta yake hivyo akawa upande wa China, Urusi, India na Ujerumani, hivyo Marekani akaanza kuwaunga mkono watu wa Darfur wadai haki yao ya ardhi.

Gaddafi na Bashir wakashirikiana vilivyo kueneza propaganda za umajumui wa Kiarabu jangwa la Sahara na hatimae kundi la wanamgambo na waasi wa Janjaweed likaanzishwa na viongozi hao ili kuwapora ardhi watu wa Darfur na kusimamia biashara zao za silaha na magendo jangwani. Kundi hilo lilipewa nguvu na jeshi la Sudan na Libya huku likifanya mauaji, ubakaji na unyanyasaji kuanzia Darfur mpaka Kordofan.




tutaendelea


Kundi hilo la Janjaweed lilianzishwa mwaka 1987 na Gaafar Nimeiry, Omar AL Bashir na Muammar Gaddafi chini ya kiongozi wao Generali Mohammed Hamdani Dagalo na Generali mdunguaji Hilal Mussa.

Kundi la Janjaweed lilianzishwa baada ya Raisi wa Chad mbabe wa vita kutoka jangwa la Sahara Generali Hissen Habrew ambaye alikuwa Raisi wa Chad kuanzia mwaka 1982_1990, Hissen Habrew alimpiga Muammar Mohammed Abu Minyar Gaddafi kwenye vita kati ya Libya na Chad hasa kipindi cha 1985_1988. Kibaraka wa Muammar Gaddafi nchini Chad Generali Sheick Omaer Saeed alikimbilia Darfur na kupokelewa na kiongozi wa makabila ya Kiarabu yaliyozamia Darfur chini ya kiongozi wao Generali mdunguaji Hilal Mussa. Baadae ndipo kundi hilo likaanzishwa.

Jeshi la Sudan na Libya waliwapa silaha na vifaa vya kijeshi waasi wa Janjaweed ili kujitanua Darfur na kupata maeneo ya kufuga pia kulinda maslahi ya makampuni yaliyokuwa yanachimba mafuta ukanda wa Darfur. Baada ya kundi hilo kuanza ugaidi na uporaji huko Darfur ndipo wazawa wa eneo hilo wakajiunganisha na kuanza vuguvugu za mapinduzi na mageuzi dhidi ya wavamizi wa Kiarabu.

Vita vya Darfur /Land Cruiser war /Vita ya Waislamu waarabu na Waislamu waafrika. 2003_2019.

Vita hii ilianza eneo la Darfur mwezi wa pili mwaka 2003 ambapo kundi la Sudan Liberation Movement (SLM) kikundi hichi kilianzishwa mwaka 2002 na makabila matatu ya waafrika kutoka Darfur hasa Fur, Zaghawa na Masalit chini ya viongozi wao Abdul Wahid AL Nur kutoka jamii ya Fur ambao ndio wenyeji na wazawa wa Darfur tangu mwaka 10,000 K.K na Minni Minnawi kutoka kabila la Zaghawa.

Kikundi cha pili kilikuwa ni Justice and Equality movement (J.E. M) kikundi hichi kilianzishwa mwaka 2000 na Khalil Ibrahim na mdogo wake Gibril Ibrahim. Vikundi vyote vya wapiganaji wa Darfur vilipata misaada kutoka kwa Marekani, Israel na Uingereza ili kupambana na serikali ya Omar AL Bashir huku kikundi cha wanamgambo wa Janjaweed kikipata vifaa kutoka Jeshi la Libya na Sudan, pia makampuni ya mafuta kutoka China yalikiunga mkono kikundi hicho cha Janjaweed (yaani ninja wa jangwani).

Vikundi hivi viliungana kwa sababu ya.... INAENDELEA....

Makala kama hizi na nyingine nyingi utazipata ndani ya Group la "Maktaba Kuu"

Utaratibu wa kuunganishwa kwenye Group la "Maktaba Kuu" ni huu ufuatao...

Namna ya kujiunga unapaswa kulipa ada "Subscription fee" Tsh 3000/= (US$ 2) tu kwa mwezi kwa namba hii +255762155025. (Jina litoke Mpoki Buyah Kaminah) baada ya kutuma pesa utaunganishwa kwenye kundi.

Kwa wale walio njee ya Tanzania wawasiliane na Mimi Whatssap +255679555526 ili kuwapa utaratibu wa kutuma ada ya kujiunga (Subscription fee).

Pamoja na Mimi, pia Kundi litakuwa na makala kutoka kwa wataalam wafuatao Lugete Gulu Maester, Mpoki Buyah  na mwalimu Mayuni Joseph.

No comments

Powered by Blogger.