JE UNAIJUA NAFASI YAKO YA KUPATA PESA
JE UNAIJUA NAFASI YAKO YA KUPATA PESA?
by maajabu blog
PESA NI NINI????????????????????????????
Pesa inatambulika kama nyenzo ya kukuwezwesha kupata
kitu au huduma, lakini kwa watu wengine huchukuliwa
katika tafsiri tofauti,Kwa wengine pesa kwao huwa ni
ulinzi na furaha na kwa wengine huwa ni starehe au njia
ya kumaliza matatizo aliyonayo huyo muhusika.
Lakini kuna upande mwingine wa Pesa, namna gani
unaweza kuipata au kuivuta ije kwako.
Hujawahi kusikia watu wakisema hata wewe ukisema
kwanini Fulani anatengeneza pesa kuliko mimi na
inawezekana wewe na yeye mumezaliwa tarehe moja na
nyota yenu ni moja.
Pamoja na kwamba nyota yako inachangia katika wewe
kupata pesa kuna mambo mengine yanaweza kukupa
mchango mkubwa katika kupata pesa mfano,sehemu
ulipozaliwa, elimu yako, makuzi ya wazazi wako, pamoja
na mambo mengine ni moja wapo ya mambo ambayo
yanachangia wewe kuwa na Uchumi mzuri au kivutio cha
Pesa.
Wakati mwingine sio wewe hata mimi huwa najiuliza ni
kwa nini watu wanaozaliwa tarehe mmoja mwezi mmoja
lakini huwa wanatofautiana mwingine tajiri na mwingine
maskini au hana kitu!!!!!.
Kwanza kabisa Jina lako ni muhimu sana, kama ilivyo
tarehe yako ya kuzaliwa katika kukusaidia wewe kupata
Mfano unampa mtoto jina Matatizo,shida au tabu
na kadhalika.
Jina huwa linaweza kubadilishwa lakini tarehe ya
kuzaliwa haibadiliki kama ilivyo Mshale wa Kampasi
ambao saa zote huwa unaelekea kaskazini………
Hii ndio sababu kila tarehe lazima iwe na maelezo yake
ya namna ya kufanya ili kuweza kupata mafanikio
Mfano Hata ukiwa umezaliwa tarehe moja na mtu
mwingine hamuezi kuugua ugonjwa mmoja au kuoa
tarehe moja na wala kuweza kupata mafanikio wakati
mmoja, kwa hiyo tofauti zilizopo za namna ya kupata
pesa ni lazima zieleweke.
UNAIJUA NAFASI YAKO YA KUPATA PESA?
Ikiwa umezaliwa tarehe 1 10, 19, 28 ya mwezi wowote Au
kama hujui tarehe yako ya kuzaliwa ikiwa jina lako
limeanzia na Herufi za (A, J, S.) wewe huwa
unazichukulia pesa kama njia ya kumaliza matatizo yako
au njia ya kuinua jina lako, hadhi yako au nafasi yako
kimaisha na katika Jamii.
Njia nzuri ya wewe kupata pesa ni kujiingiza katika
Nyanja au kazi ambazo ni mpya na halisi au za uhakika
, kwa maana ya kufanya Biashara mpya kuwa na miradi
mingi kwa wakati mmoja au huku unafanya kazi huku
unafanya biashara.
Kama ilivyo tarehe yako ya kuzaliwa unatakiwa uwe na
mamlaka juu ya wengine kwa maana ya kwamba uwe
wewe ndie mmiliki wa shughuli, kama kampuni yako
mwenyewe na siyo kuajiriwa au kutumwa
Jitegemee, jitume na uwe ni wewe, jaribu kuwa na hisia
au mawazo ya kufanikiwa na mara kwa mara buni njia
tofauti za kupata pesa tena nyingi.Jaribu kuwa
muaminifu na kopa katika Taasisi zinazoeleweka. Miezi
ya Februari, April na Agosti ndio miezi yako ya
mafanikio,katika utekelezaji wa Shughuli zako jaribu
sana kuwa makini na mfuatiliaji wa mambo yako
usiwaachie watu. Tahadhari katika miezi ya Januari, May
na Oktoba, hii siyo miezi mizuri kwako usikope wala
kukopesha au kuanzisha shughuli yoyote ya kipato
katika miezi hiyo.
Waliofanikiwa katika kipengele hiki ni kama hawa
wafuatao:-
1. Dolly Patron alizaliwa tarehe 19/1/1964
2. Rod Stewart alizaliwa tarehe 10/1/1945
3. Lee Marvin alizaliwa tarehe 19/2/1964
4. Jacqueline Kennedy onasis alizaliwa tarehe 28/2/1926
5. Lisa marie Presley alizaliwa tarehe 1/2/1929
6. Bruce willis alizaliwa tarehe 19/3/1955
7. Evander holyfield alizaliwa tarehe 19/10/1962
8. William Bill Gate alizaliwa tarehe 28/10/1955
9. Ted Turner alizaliwa tarehe 19/11/1938.
WATU WA NAMBA MBILI
Ikiwa umezaliwa tarehe 2 11, 20, 29 ya mwezi wowote
Au kama hujui tarehe yako ya kuzaliwa ikiwa jina lako
limeanzia na Herufi za (B, K, T.) Wewe huwa unakuwa
na aibu katika utafutaji wa Pesa hasa katika shughuli
zako mwenyewe.
Njia nzuri sana kwako wewe kupata pesa ni kwa
kuzikusanya na kuzihifadhi kidogo kidogo kwa muda
mrefu, kwako wewe kinyota huwezi kupata pesa nyingi
kwa wakati mmoja na huwa
zinakuja ukiwa unajishughulisha na shughuli
zinazohusiana na jamii, mambo ya ubunifu, mbinu na
mipango ya watu ambao mnaelewana au wako tayari
kushirikiana na wewe, hiyo itakuongezea spidi ya wewe
kupata pesa.
Jiunge katika kusaidia watu hiyo itakuletea faida ya
kifedha baadae, Biashara ya kununua na kuuza itakupa
faida kubwa. Shughuli zako za kipato kubwa zifanyike
kwa ushirikianao na watu waliozaliwa Mwezi January, May, July na Oktober
Kuwa na tahadhari kukopa pesa au kujiingiza katika
biashara miezi ya April, November na Januari.
Waliofanikiwa ambao ni Mamilionea katika kipengele hiki
ni kama hawa wafuatao:-
1. Oprah Winfrey alizaliwa tarehe 20/1/1954
2. Michael Jackson alizaliwa tarehe 29/8/1958
3. Spike lee alizaliwa tarehe 20/3/1957
4. Cindy Crawford alizaliwa tarehe 20/2/1966
5. Andre Agassi alizaliwa tarehe 29/4/1970
WATU WA NAMBA TATU
Ikiwa umezaliwa tarehe 3 12, 21, 30 ya mwezi wowote
Au kama hujui tarehe yako ya kuzaliwa ikiwa jina lako
limeanzia na Herufi za (C, L, U.)
Wewe ni mtu ambaye huwa unaishi kwa wakati huo uliopo, kwa maana unatumia unachokipata kila
kinapokuja, hali hii inakufanya utumie hata akiba yako
uliyonayo au mtaji wako ulionao. Njia nzuri ya
kukufanya uwe na pesa nyingi ni kujithibiti, Ukifikiri
makubwa basi utafanikiwa pakubwa, neno kushindwa
lisiwe lako, ukiwa na tabia ya kujiamni utafanikiwa sana.
Kopa, kuwa muaminifu na lipa madeni yako kwa wakati,
muda mzuri wa wewe kupata pesa ni Mwezi wa March,
May, Oktober na Decemba, miezi ambayo unaweza
kupata matatizo ya kifedha ni mwezi wa February, June
Agosti na September
Waliofanikiwa ambao ni Mamilionea kwa kipengele hiki
ni hawa wafuatao:-
1. Bill Cosby alizaliwa tarehe 12/7/1937
2. Mike Tyson alizaliwa tarehe 30/6/1966
3. Eddie Murphy alizaliwa tarehe 3/4/1961
4. Mel Gibson alizaliwa tarehe 3/1/1956
5. Tiger Woods alizaliwa tarehe 30/12/1975
WATU WA NAMBA NNE
Ikiwa umezaliwa tarehe 4 13, 22, 31 ya mwezi wowote
Au kama hujui tarehe yako ya kuzaliwa ikiwa jina lako
limeanzia na Herufi za (D, M, V.)
Wewe ni mmoja ya watu ambao unaweza au unapata pesa
zako kwa wingi sana katika njia ambao si za kawaida.
Kuna wakati unaweza ukawa na pesa nyingi sana na kuna
wakati unakuwa huna kitu kabisa. Unaweza kuwa
tofauti na pesa lakini una njia ya kuzitumia unapozipata
unatakiwa ili kuhifadhi hizo pesa uishi kwa kuwa na
rekodi nzuri ya fedha, bajeti nzuri na matumizi yako
yaendane na kipato chako, unapofanya manunuzi jaribu
kulilia hali, nunua vitu vya bei ya chini na utapata
Maendeleo Makubwa katika pesa.
Biashara na masuala ya kipato yafanyike mwezi wa
Februari, June, na Agosti , miezi mibaya kwako kifedha
ni mwezi wa January, May na Oktoba.
Waliofanikiwa ambao ni Mamilionea kwa kipengele hiki ni
hawa wafuatao:-
1. Stevie Wonder alizaliwa tarehe 13/5/1950
2. Clint Eastwood alizaliwa tarehe 31/5/1966
3. Wesley Snipes alizaliwa tarehe 31/7/1962
4. Naomi Campbell alizaliwa tarehe 22/5/1970
5. Dennis Rodman alizaliwa tarehe 13/5/1964
WATU WA NAMBA 5
Ikiwa umezaliwa tarehe 5 14, 23, ya mwezi wowote Au
Ikiwa umezaliwa tarehe 5 14, 23, ya mwezi wowote Au
kama hujui tarehe yako ya kuzaliwa ikiwa jina lako
limeanzia na Herufi za (E,N, W.)
Wewe ni mtu ambaye unapenda kuishi kwa wakati, (kwa
maana ya kutumia kilichopo kulingana na hali yako), hali
hii au tabia hii uliyonayo huathiri sana kipato chako.
Huna tabia nzuri ya kuhifadhi fedha. Wewe ni mtu
ambaye unaweza kupata fedha kwa kufanya majaribio,
bila ya kuwa na tahadhari (Usiwe muoga) na kwa
kubahatisha.
Ukiwa na shughuli zaidi ya moja inaweza kukusaidia sana
kupata pesa za ziada
Kwa vile number 5 ni namba ya Habari na Matangazo,
jitangaze na sana jiuze kwa kutumia Radio, Televisheni,
Magazeti utapata mafanikio makubwa.
Ukikumbuka kujilipa wewe kwanza kabla hujawalipa
wengine utaona kwamba kipato chako kitakuwa sana na
kwa haraka.
Mafanikio yako ya kipesa huwa yanapatikana Sana mwezi
wa February, May na June na miezi mibaya kwako kipesa
ni mwezi wa January, March na December
Waliofanikiwa ambao ni Mamilionea kwa kipengele hiki ni
hawa wafuatao:-
1. Julio iglesias alizaliwa tarehe 23/9/1944
2. Michael Caine alizaliwa tarehe 14/3/1933
3. Prince Charles alizaliwa tarehe 14/11/1948
4. Quincy Jones alizaliwa tarehe 14/3/1933
5. Colline Powell alizaliwa tarehe 5/4/1937
WATU WA NAMBA 6
Ikiwa umezaliwa tarehe 6 15, 24, ya mwezi wowote Au
kama hujui tarehe yako ya kuzaliwa ikiwa jina lako
limeanzia na Herufi za (F,O, X.)
Njia nyepesi kabisa ya wewe kupata mafanikio ya kipesa
ni kujituma kuwajibika kwa matendo yako, kwa maana
mafanikio yanakuwa yako, kukosa kwako ni jambo la
kawaida na mapingamizi kwako iwe ni changamoto ya
kujituma zaidi na sio kukata tamaa.
Njia nyingine uliyonayo ya kupata pesa ni kuwa una hisia
ya thamani unajua thamani ya pesa, unapokuwa unafanya
biashara unakuwa asilia kwa maana biashara iko ndani ya
damu yako, unaweza ukamuuzia mtu kitu hata kama
hakitaki na unaweza kulilia hali pale inapotakiwa.
Kwa vile namba hii ni ya ushirika au ushirikiano
utafanikiwa sana ukiwa utawashirikiasha wenzio katika
mambo yako usifanye mambo peke yako
Hata hivyo fikra za kutokufanikiwa au kuwa na wasiwasi
kwamba watu watakufikiriaje zinaweza kukuzuia usipate
utajiri.
Fanya masuala ya kipesa mwezi wa Machi, May, July na
Oktoba. Jaribu sana kuepuka miezi ya Februari, Aprili na
Agosti
Waliofanikiwa ambao ni Mamilionea kwa kipengele hiki ni
hawa wafuatao:-
1. Sylvester Stallone alizaliwa tarehe 23/9/1944
WATU WA NAMBA 7
Ikiwa umezaliwa tarehe 7 16, 25, ya mwezi wowote Au
kama hujui tarehe yako ya kuzaliwa ikiwa jina lako
limeanzia na Herufi za (D, M, V.)
Wewe ni mtu ambaye pesa zako hupatikana kwa pole
pole na umakini mkubwa.ili kupata hayo mafanikio ya
kipesa, Unatakiwa uwe una uelewa mkubwa katika
utafutaji wa pesa, kwa maana kwamba uwe unajua
unafanya nini au unataka kufanya shughuli gani katika
kutafuta pesa. Jambo hilo litakusaidia sana katika kujua
pesa utazipataje.
Katika utafiti wangu wa mamilionea sikushangaa sana
kuona kwamba wale wote waliozaliwa katika namba 7
wamekuwa ni watu wa nyuma nyuma au wenye aibu
katika utafutaj pesa. Hasa ikizingatiwa kwamba namba
saba ni namba ya kiroho na kimungu na siyo ya kidunia .
Ukitaka mafanikio ya kipesa ni lazima uwe na Ubunifu na
utambuzi wa nini unataka, hali hiyo itakusaidia sana kwa
uwezo wa juu kuvutia mambo yote yanayohusiana na
wewe kupata pesa.
Yaweke pembeni na usiyaone kabisa yale ya kidunia
ambayo yanaweza kukusababishia wewe kupoteza fedha
hata zikiwa kidogo, Tumia mbinu zako na uelewa wako
ambao umeupata kwa miaka mingi, ukiwa katika hali hii
itakusaidia sana kuweke kupata mafanikio,
Kwa vile dunia ya sasa ni ya khabari na teknologia tumia
uwezo wako katika hayo na utaona mafanikio makubwa
Muda mzuri wa wewe kufanya biashara ni miezi ya May,
July, na Agosti na miezi mibaya ya kifedha ni Januari,
April na November.
Waliofanikiwa ambao ni Mamilionea wa kipengele hiki ni
hawa
wafuatao:-1. Kareem Abduljabar alizaliwa tarehe 16/4/1947
2. Sean Connery alizaliwa tarehe 25/8/1930
3. Madonna alizaliwa tarehe 16/8/1958
4. Will Smith alizaliwa tarehe 25/9/1968
5. Elton John alizaliwa tarehe 25/3/1947
6. John F Kennedy Jr alizaliwa tarehe 25/11/1960
7. David Copperfield alizaliwa tarehe 16/9/ 1956
8. Nicholas Cage alizaliwa tarehe 7/1/1964
No comments